IQNA

Ustadh Abdul Basit akumbukwa

13:16 - December 03, 2012
2
Habari ID: 2457829
Shughuli ya kumkumbuka karii mashuhuri wa Qur’ani Ustadh Abdul Basit Abdul Samad ilifanyika Ijumaa iliyopita nchini Misri ikihudhuriwa na makarii na wapenzi wa Qur’ani Tukufu.
Wanafunzi na wapenzi wa karii huyo mashuhuri wa Qur’ani, wanachama wa Jumuiya ya Masomaji Qur’ani ya Misri na shakhsia wakubwa kama Sheikh Mahmoud Tablawi, Mahmoud Siddiq Minshawi, Muhammad al Halbawi, wawakilishi wa Kituo cha Kiislamu cha al Azhar na Wizara ya Wakfu ya Misri na mabalozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu nchini humo pia wameshiriki katika shughuli hiyo ya kumbkumbuka karii mashuhuri wa ulimwengu wa Kiislamu.
Ustadh na karii mashuhuri wa Qur'ani Abdul Basit Muhammad Abdul Samad aliaga dunia tarehe 30 Disemba mwaka 1988 katika mji mkuu wa Misri, Cairo.
Alianza kujifunza Qur'ani Tukufu akiwa bado mtoto mdogo na alipewa tuzo ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani akiwa na umri wa miaka 12. Kipindi fulani Ustadh Abdul Basit alitumia muda wake mwingi kusafiri katika nchi za Kiislamu na kuwahamasisha watu kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu.
Ustadh Abdul Basit ameacha kanda nyingi za Sauti ya kiraa yake ya Qur'ani Tukufu ambazo bado zinawavutia wasomaji wengi wa Qur'ani.
Imechapishwa: 2
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
shekh salum Ahmada Salum
0
0
Alieanza kaanza na atadumu na kutamkwa
Tufateni nyayo zake
shekh salum Ahmada Salum
0
0
Alieanza kaanza na atadumu na kutamkwa
Tufateni nyayo zake
captcha