IQNA

Makundi ya Kiislamu ya Misri kufanya maandamano kesho

11:43 - December 10, 2012
Habari ID: 2461173
Makundi ya Kiislamu ya Misri yanafanya maandamano kesho kumuunga mkono wito wa kiongozi wa nchi hiyo wa kufanyika kura ya maoni kuhusu rasimu ya katiba mpya ya nchi hiyo.
Msemaji wa kundi la Ikhwanul Muslimin Mahmoud Ghazlan amesema kuwa maandamano hayo yatafanyika kwa kaulimbiu ya suluhu ya kitaifa.
Wakati huo huo wapinzani wa Mursi pia wanapanga kufanya maandamano ya kupinga kura hiyo ya maoni.
Rais Muhammad Mursi wa Misri jumamosi iliyopita amebatilisha dikrii ya kujiongezea madaraka.
Taarifa iliyotolewa na kiongozi huyo kwa vyombo vya habari imesema kwamba dikrii kuhusu katiba imebatilishwa kwa sasa lakini kura ya maoni ya rasimu ya katiba itafanywa kama ilivyopangwa hapo Disemba 15.
Novemba 22 Rais Muhammad Mursi alitangaza dikrii iliyovivua vyombo vyote vya sheria nchini Misri uwezo wa kuvunja Bunge la Katiba, ambalo lilikuwa likitunga rasimu ya katiba mpya.
Dikrii hiyo pia ilimpa Rais uwezo wa kuchukua hatua yoyote ili kulinda mapinduzi suala lililoonekana kama kwamba amejiongezea madaraka. Tangu wakati huo Misri ilikumbwa na ghasia na machafuko ya kupinga dikrii hiyo.
1150864
captcha