Ayatullah Mohsen Araki, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kuyakurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu amesema leo kuwa, Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran atahudhuria pia mkutano huo uliopangwa kufanyika tarehe 27 hadi 28 mwezi huu hapa mjini Tehran.
Ayatullah Araki ameongeza kuwa, jumla ya wanafikra elfu moja kutoka Iran na wanasayansi watajika, wanasiasa na shakhisia wa kisiasa 300 wa ulimwengu wa Kiislamu wakiwemo wanafikra kutoka Chuo Kikuu cha al Azhar cha Misri, Mamufti wakuu wa Sudan, Tunisia na Syria pamoja na wanafikra kutoka Pakistan na nchi za eneo la Ghuba ya Uajemi ni miongoni mwa washiriki wa mkutano huo wa kimataifa wa Umoja wa Kiislamu.
1174593