IQNA

Idadi ya Wafaransa wanaosilimu yaongezeka mara dufu

19:47 - February 18, 2013
Habari ID: 2498647
Afisa anayeshughulikia masuala ya dini katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ufaransa amesema kuwa idadi ya watu wanaoingia katika dini ya Uislamu imeongezeka mara dufu nchini humo katika kipindi cha miaka 25 iliyopita.
Bernard Godard amebainisha suala hilo katika ripoti iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ufaransa na kuongeza kuwa, suala la watu kuingia katika dini ya Uislamu nchini Ufaransa limekuwa jambo muhimu na kwamba ongezeko la idadi ya watu wanaoingia katika dini hiyo nchini humo hususan mwaka 2000 ni jambo linalohitaji kupewa mazingatio.
Duru mbalimbali zinasema mwenendo mzuri wa Waislamu wa Ufaransa katika masuala mbalimbali ya kijamii na kiutamaduni ndio unaowavutia Wafaransa wengi katika dini ya Uislamu licha ya propaganada chafu zinazofanywa na vyombo vya habari dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Wafaransa milioni sita ni wafuasi wa dini ya Kiislamu na Wafaransa kati ya laki moja hadi mbili wameingia katika dini hiyo.
Takwimu hizo zinaonesha kuwa idadi ya Wafaransa wanaoingia katika dini ya Uislamu tangu mwaka 2000 imeongezeka mara dufu ikilinganishwa na ile ya mwaka 1986 ya watu laki tano pekee kwa mwaka. 1190623
captcha