IQNA

Wabahrain waandamana kupinga mashindano ya langa-langa (F1)

13:43 - April 21, 2013
Habari ID: 2521926
Vikosi vya kijeshi Bahrain vimetumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji wanaopinga kufanyika mashindano ya magari ya langa-langa ya Formula One Grand Prix ambayo yanatazamiwa kuanza leo katika mji mkuu, Manama.
Watu wa Bahrain wanataka mashindano hayo yasimamishwe kwa sababu utawala wa ukoo wa Aal Khalifa unakandamiza maandamano ya amani ya wanaotaka mabadiliko nchini humo. Wabahrain wanasema utawala wa kifalme unataka kutumia mashindano hayo ya langa-langa kuonyesha kila kitu ni shwari katika nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi.

Kwa miaka miwili sasa Bahrain imekumbwa na mgogoro mkubwa uliosababisha mashindano hayo ya magari yasifanyike mwaka 2011. Mwaka 2012 utawala wa Aal Khalifa ulifanya mashindano hayo kwa kustafidi na uungaji mkono wa vikosi vya usalama vya Saudia. Lakini mwaka huu wananchi na wapinzani wa Bahrain wamesisitiza kuendelea na malalamiko yao dhidi ya hatua kama hizo za kimaonyesho, licha ya ukandamizaji wa utawala wa kifalme wa Aali Khalifa.
Wapinzani wa nchi hiyo wameitaka jamii ya kimataifa badala ya kushiriki kwenye mashindano hayo ya mbio za magari ilaani ukiukwaji haki za binadamu na ukandamizaji wa utawala wa Bahrain na kuunga mkono matakwa ya wananchi yanayodhihirishwa kwa maandamano ya amani kwa kususia mashindano hayo.
1215836
captcha