Seyyed Nasrallah aliyasema hayo Jumamosi katika sherehe za kuadhimisha mwaka wa 13 wa kuondoka kwa madhila vikosi vya utawala haramu wa Israel kusini mwa Lebanon. Siku hiyo huadhimishwa kama Siku ya Ukombozi nchini Lebanon.
Kiongozi wa Hizbullah amesema iwapo magaidi wanaopata himaya ya kigeni nchini Syria watashinda, wanakusudia kutumia silaha zao dhidi ya Lebanon.
Seyyed Nasrallah pia ameashiria makundi yenye misimamo mikali ya Kiwahabbi ambayo ndiyo uti wa mgono wa machafuko Syria na kusema makundi hayo yanayopata uungaji mkono wa Marekani ni tishio kwa jamii zote nchini Lebanon. Kiongozi wa Hizbullah amebainisha kuwa vita dhidi ya serikali ya Syria ni sehemu ya mradi wa Marekani wa kubadlisha mlingano wa nguvu katika eneo la Mashariki ya Kati kwa maslahi ya utawala haramu wa Israel. Seyyed Nasrallah amesema hatimaye Mujahidina wanaopigana dhidi ya Mawahabbi watapata ushindi nchini Syria.
1233572