IQNA

Rais Rouhani: Serikali ziache kuunga mkono ugaidi

20:45 - December 09, 2014
Habari ID: 2617107
Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema, madola yanayounga mkono ugaidi yanapaswa kuacha kutoa misaada yao ya moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja kwa magaidi na badala yake yashirikiane na waathirika wa ugaidi.

Rais Rouhani ameyasema hayo katika hotuba yake ya kufungua rasmi Kongamano la Kimataifa la Ulimwengu Dhidi ya Misimamo Mikali na Utumiaji Mabavu hapa Tehran. Rais Rouhani ameongeza kuwa madola ambayo yamekuwa yakiunga mkono ugaidi sasa yanapaswa kutoa msaada wa kifedha, kiintelijensia na kijeshi kwa nchi ambazo zinakabiliwa na hujuma za kigaidi. Ameongeza kuwa Iraq na Syria zimetumbukizwa katika maafa makubwa ya kibinaadmau na hivyo serikali ambazo zimeunga mkono magaidi katika nchi hizo mbili zinapaswa kuchukua jukumu la kulipa fidia kwa waathirika. Rais Rouhani pia ametoa mwito wa kuwepo ushirikiano wa kieneo kwa lengo la kubadilisha mfumo wa masomo ili kukabiliana na tafsiri zinazochochea misimamo mikali katika mafundisho ya kidini. Rais Rouhani pia amelikosoa vikali Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kushindwa au kuzembea kukabiliana na vitisho dhidi ya amani na usalama wa kimataifa. Ameutaka Umoja wa Mataifa kubeba jukumu kubwa zaidi katika vita dhidi ya ugaidi. Kongamano hilo limehudhuriwa na maafisa wa kisiasa, wasomi na wajumbe mbalimbali kutoka nchi za Afrika, Asia na Amerika ya Latini.../mh

2616891

captcha