IQNA

Al Azhar: Jihadi dhidi ya Daesh (ISIL) ni wajibu

17:56 - December 12, 2014
Habari ID: 2617813
Kituo cha Kiislamu cha al Azhar nchini Misri kimetoa wito wa kufukuzwa magaidi wote katika nchi za Waislamu.

Wito huo ulitolewa jana na Kituo cha Kiislamu cha Azhar katika mkutano uliofanyika mjini Cairo kuchunguza njia za kisheria za kupambana na makundi ya kigaidi.

Al Azhar imesema makundi ya kigaidi kama lile la Daesh (ISIL) na Ansar Baitul Muqaddas yamepuuza wito wa kuimarishwa umoja miongoni mwa Waislamu na hamu yao kubwa ni kutwaa madaraka kwa kutumia mabavu na yanatumia dini kama wenzo wa kufikia malengo yao.

Al Azhar ya Misri imesisitiza kuwa, watawala wa jamii za Waislamu wanapaswa kuchukua hatua za kuwaadhibu wale wote wanaohusika na mauaji ya watu wasio na hatia.

Makundi ya kigaidi kama lile la Daesh yaliyoanzishwa kwa msaada wa nchi za Magharibi kama Marekani na washirika wao wa Mashariki ya Kati yamekuwa yakifanya mauaji makubwa dhidi ya raia katika nchi za Syria na Iraq na kubomoa maeneo matukufu ya kidini ikiwa ni pamoja na kuvunja makaburi ya Mitume wa Mwenyezi Mungu na masahaba wa Mtume Muhammad (saw).../mh

2617385

captcha