Sheikh Adnan Qassem Salehi ambaye yuko katika jopo la majaji wa Mashindano ya Tano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wanachuo Waislamu amesema mashindano kama hayo ambayo yanafanyika kwa kiwango cha kimataifa pia yanatoa msukuomo kwa Waislamu kuweza kuwasilisha taswira sahihi ya Uislamu duniani.
Ameongeza kuwa mashindano hayo halikadhalika yanastawisha Umoja wa Kiislamu mbali na kuarifisha mafundisho ya Ahul Bayt AS. Msomi huyo wa Iraq pia amewashukuru walioandaa mashindano hayo.
Mashindano ya Tano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wanachuo Waislamu yanaaza leo Alkhamisi katika ukumbi wa Mnara wa Milad katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Tehran. Mashindano hayo ya siku nne yana washiriki 66 kutoka nchi 47 ambao ni wanafunzi wa vyuo vikuu na watashindana kusoma (qiraa) na kuhifadhi Qur'ani Tukufu.../mh