IQNA

Waueni na wanyongeni Daesh, wameondoka katika dini

17:04 - February 04, 2015
Habari ID: 2809497
Sheikh Mkuu wa al Azhar nchini Misri Ahmad al Tayyib ametoa taarifa akilaani kitendo cha kundi la kigaidi la Daesh cha kumchoma moto akiwa hai rubani Moaz al-Kassasbeh wa Jordan. Amekitaja kitendo hicho kuwa ni cha kigaidi na kishetani.

Sheikh wa al Azhar amesema Uislamu umekataza kuua nafsi isiyo na hatia na imeharamisha kuchoma moto nafsi katika hadhara au kwa njia yoyote ya kidhalimu hata katika vita na adui mvamizi. Amesema kitendo cha kundi la Daesh ni uovu unaopigwa vita na dini zote
Tarifa ya Sheikh Mkuu wa al Azhar imesema wanachama wa Daesh ni mafisadi na waharibifu katika ardhi ambao wanapigana vita dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kwa msingi huo wanapaswa kuadhibiwa. Sheikh al Tayyib ameitaka jamii ya kimataifa kukabiliana vilivyo na kundi hilo la kigaidi lililofanya jinai za kutisha. AIR  2808398

captcha