Duru zinaarifu kuwa amri hiyo imetolewa na wakuu wa Daesh katika mji wanaoukalia kwa mabavu wa Mosul nchini Iraq. Ismat Rajab, afisa wa Chama cha Kidemokrasia cha Kurdistan (KDP) ameviambia vyombo vya habari kuwa kundi hilo la kigaidi limewaonya wakaazi wa Mosul wasithubutu kusali sala ya Idul Fitr. Kundi la Kitakfiri la Daesh limedai kuwa sala ya Idul Fitr si ya Kiislamu na ni bidaa. Kundi hilo limeendelea kudai kuwa, ‘Sala ya Idul Fitr kiasili si ya Kiislamu’ tokea wakati wa awali wa kudhihiri Uislamu.
Mosul, mji mkubwa zaidi ulio chini ya Daesh nchini Iraq, ulikuwa na watu takribani milioni mbili kabla ya hujuma ya Matakfiri wa Daesh mwaka jana. Matakfiri hao wa pote la Kiwahabbi wameleta sheria zenye misimamo mikali ya kidini ambazo zimepingwa na kukoselwa na maulamaa wa Kiislamu duniani. Matakfiri hao pia wamebomoa maziara matakatifu na misikiti ya Masunni na Mashia katika maeneo wanayoshikilia Iraq na Syria. Kundi la kigaidi la ISIS linaaminika kuundwa na mashirika ya kijasusi ya Saudi Arabia, Utawala haramu wa Israel na Marekani.../mh