Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mahafali hiyo ya qiraa na tilawa ya Qur'ani lilifanyika Julai 12 katika Masjidul Quds mjini Cape Town ambapo wa kwanza kusoma alikuwa Qari Mahmoud Abdulwahab Tantawi na baada yake akasoma qarii Muiraqi Raafie Al Amiree.
Aidha katika mahafali hiyo ya Qur'ani, qarii Mohammad Safar wa Sudan, qarii mashuhuri wa Misri Dakta Sheikh Farajallah Mahmoud Shadhili wa Misri na Qarii Ustadh Azraie bin Abdul Haq wa Malaysia walisoma aya za Qur'ani Tukufu. Aidha kulikuwa pia na maqarii kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Algeria.
Tamasha la Kimataifa la Qur'ani Tukufu limemalizika kwa kutunukiwa zawadi na cheti washiriki wote.../mh