Sa’ad Dawabsheh, aliyekuwa na umri wa miaka 32 na baba yake Ali, amefariki mapema leo Jumamosi katika kituo cha afya ya Soroka katika mji wa Beersheba kusini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Israel. Dawabesh alipata majeruhi ya asilimia 80 siku chache zilizopita wakati walowezi Waisraeli walipovamia na kuitetekeza nyumba alimokuwa na familia yake katika eneo la Ukingo wa Magharibi. Mke wake, Rihan na mtoto wao wa miaka minne, Ahmad wako katika hospitali hiyo na hali yao ni mahututi. Ikumbukwe kuwa Julai 31 mtoto wa miezi michache Palestina aliuawa kwa kuchomwa moto na Waisreali waloweziwa Kizayuni ambao walivamia nyumba alimokuwa na kuiteketeza moto katika eneo linalokaliwa kwa mabavu na Israel la Ukingo wa Magharibi. Jamii ya kimatiafa inaendele akulaani vikali ugaidi huo wa Waisraeli dhidi ya mtoto huyo mchanga wa Palestina na familia yake.../mh