Mkuu wa Kamati ya Jimbo ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Majukumu Maalumu, Ghazali Taib amesema tayari misingi ya awali imeshawekwa kuanzisha chuo hichi.
“Tayari tuna Taasisi ya Darul Qur’an ambayo itapandishwa hadhi na kuwa chuo kikuu,” amesema Taib.
Ameongeza kuwa kuanzishwa chuo kikuu cha Qur’ani Terengganu ni pendekezo la Waziri wa Elimu Malaysia Datuk Seri Idris Jusoh ambaye aliliwasilisha wakai akiwa Waziri Mkuu wa jimbo la Terengganu.
Malaysia ni nchi iliyo katika eneo la kusini mashariki mwa Asia na takribani asilimia 65 ya wakaazi wake milioni 31 ni Waislamu.../mh