Kwa mujibu wa tovuti ya hqmi.org, mashindano hayo ya Qur’ani yamefanyika kwa himaya ya taasisi ya kidini na Qur’ani ya Hassan bin Thabit katika huko Morisi
kwa ushirikiano na Jumuiya ya Kimatiafa ya Kuhifadhi Qur’ani Tukufu.
Katika mashindano hayo yaliyofanyika katikaKituo cha Utamaduni na Kiislamu katika Kisiwa cha Morisi, washiriki walishindano katika kuhifadhi Qur’ani kikamilifu, Juzuu 15, Juzuu 3 na Juzuu 1.
Katika mashindano hayo yaliyofanyika Jumatano iliyopita kulifanyika sherehe za kuwatunuku zawadi waliopata nafasi za juu ambapo kati ya waliohudhuria ni Waziri Mkuu wa Morisi Anerood Jugnauth mbunge Ahmad Bashir Jahangeer, maulamaa na waalimu wa Qur’ani pamoja na wawakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur’ani Tukufu.
Waliozungumza katika hafla hiyo walisisitiza umuhimu wa Waislamu kutekeleza mafundisho ya Qur’ani.
Morisi ni kisiwa kilicho katika Bahari ya Hindi kusini mwa Afrika takriban 900 km mashariki kwa Madagaska na 4000 km kusini-magharibi kwa Bara Hindi. Waislamu ni takribani asilimia 20 ya idadi ya watu takribani milioni mbili na laki tatu.../mh