Salman amelizuia shirika hili kuchukua kandarasi yoyote ya ujenzi na kumwamuru waziri wa fedha wa Saudia kuangalia upya kandarasi lilizo nazo hivi sasa shirika hilo la Binladin.
Kwa mujibu wa amri hiyo, maafisa wote waandamizi wa shirika hilo pamoja na wajumbe wa bodi ya Bin Ladin Group wamepigwa marufuku kusafiri nje ya Saudia mpaka uchunguzi kuhusu ajali hiyo utakapokamilika.
Kamati ya kuchunguza ajali hiyo imetoa ripoti na kusema katika sehemu moja ya ripoti yake kuwa, shirika la Bin Ladin Group linapaswa kulaumiwa kwa namna fulani, kutokana na ajali hiyo ya kutisha.
Mfalme wa Saudia pia ametoa amri ya kulipwa dola 267,000 kwa kila familia ya wahanga wa ajali hiyo na karibu ya nusu ya fedha kama hizo watalipwa mahujaji waliojeruhiwa.