IQNA

Mfalme wa Saudia aamuru kanda za kamera zote za Mina zifichwe

11:16 - September 28, 2015
Habari ID: 3372681
Mfalme Salman wa Saudi Arabia ametoa amri ya kukusanywa kanda zote za kamera zilizosajili maafa ya kusikitisha ya Mina.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA aliyenukulu kutoka tovuti ya mepanorama, Mfalme  salman ametoa amri ya kukusanywa kande zote za kamera zilizosajili maafa ya Mina na kwamba kanda hizo  ziwekwe mahala pa siri.
Amri hiyo inatolewa katika hali ambayo Waislamu duniani wanataka iundwe kamati ya kimataifa kuchunguza maafa ya Mina. Ni kwa sababu hiyo ndio watawala wa Saudia wanafanya kila wawezalo kukusanya yaliyomo katika kamera hizo ili ukweli usibainika.
Wakati huo huo Mwanaharakati mashuhuri wa nchini Saudia amefichua kwamba, maafisa wa usalama wa nchi hiyo walifanya makusudi katika kuzuia maafa ya Mina. Mwanaharakati huyo ambaye anatambulika kwa jina la Mujtahid ambaye amejipatia umaarufu kwa kufichua habari za siri za ndani ya ukoo wa Aal Saud, ameyasema hayo kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba, maafisa wanaosimamia ibada ya hija katika eneo la Mina walifahamua masaa mawili kabla ya kutokea maafa hayo juu ya kuwepo mrundikano wa watu lakini hawakuchukua hatua yoyote ile. Amesisitiza kuwa, ni baada ya kujiri maafa ndipo maafisa hao wakaanza kuchakarika huku na huko. Kwa mujibu wa mwanaharakati huyo, kamera ambazo zimefungwa eneo hilo zilionyesha wazi mrundikano mkubwa wa watu kabla ya kutokea maafa ambapo kulikuwepo uwezekano mkubwa wa kuzuilika janga hilo. Amesema kuwa, ni wajibu kwa utawala wa Saudia kubeba dhima ya tukio hilo chungu.
Hadi sasa inakadiriwa kuwa  mahujaji 2,000 walipoteza maisha katika msongamano mkubwa wa Mina.../mh

3372250

captcha