IQNA

Mfalme wa Saudia mahututi hospitalini

18:45 - October 06, 2015
Habari ID: 3382527
Imedokezwa kuwa Mfalme Salman bin Abdulaziz wa Saudi Arabia amelazwa hospitalini mjini Riyadh na sasa yuko katika hali mahututi.

Duru za kuaminika zimeliambia shirika la habari la Kiarabu la al-Ahd kuwa Mfalme Salman sasa yuko katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi katika Hospitali Maalumu ya King Faisal mjini Riyadh.
Duru zinadokeza kuwa kutokana na hali yake mbaya kiafya, maafisa wa Saudia wamehofia kumpeleka kwa ndege katika hospitali za Marekani.
Mfalme Salman mwenye umri wa miaka 80 anaaminika kuugua ugonjwa wa kupoteza fahamu wa Alzheimer na kwamba ufalme wa Saudia kimsingi unaendeshwa na Mrithi wa Kitu cha Ufalme, Mwanamfalme Muhammad bin Nayef. Mashahidi wanasema mfalme huyo wa Saudia huwa anapoteza fahamu mara kwa mara na anaweza kusahau alichokisema dakika chache zilizopita au watu ambao amewajua umri wake wote.
Aidha duru karibu na ufalme wa Saudia zinadokeza kuwa, mfalme huyo amepata matibabu hospitalini mara kadhaa katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita.../mh

3382398

captcha