IQNA

Kiongozi Muadhamu

Misafara ya Arubaini ya Imam Hussein AS ni dhihirisho la mahaba, imani

19:52 - November 30, 2015
Habari ID: 3458796
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema harakati iliyojaa mahaba na imani ya watu wa nchi mbali mbali za dunia katika siku ya Arubaini ya Imam Hussein AS ni moja kati ya ishara za Mwenyezi Mungu.

Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo katika kikao chake cha darsa za kharij za fiqhi mjini Tehran amesema tukio la aina yake la harakati adhimu na iliyojaa maana ya msafara mkubwa wa Aurabaini ya Imam Hussein AS ni tukio zuri na lenye kudumu. Ameongeza kuwa, ‘Mahaba na Imani’ na ‘Akili na Hisia za Ukarimu’ ni moja kati ya sifa za kipekee za mafunzo ya Ahul Bayt Alayhim Salam. Ayatullah Khamenei ameashiria kuhusu ukaribu na mahaba ya watu wa Iraq katika kuwakirimu wafanya ziara ya siku ya Arubaini huku akiwanasihi wale ambao wanapata taufiki ya kushiriki katika harakati hiyo iliyojaa maana waitumie vizuri. Ameongeza kuwa fursa ya kuwa na uhusiano wa kimaanawi na Ahul Bayt wa Mtume SAW na kuwazuru katika msafara mkubwa wa Arubaini ni moja ya sifa za kipekee za mafunzo za Ahul Bayt AS.

Majlisi za siku ya Arubaini hufanyika kila mwaka baada ya kupita siku Arubaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram kwa ajili ya kukumbuka mauaji ya mjukuu wa Mtume Imam Hussein AS na masahaba zake ambao walitoa roho zao kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika jangwa la Karbala.

3458476

captcha