IQNA

Mwanaharakati wa Kiislamu afa akiwa jela Nigeria

14:47 - January 03, 2016
Habari ID: 3470010
Harakati ya Kiislamu ya Nigeria jana ilitangaza kuwa Abbas Isiyaku mmoja wa wanachama wa harakati hiyo ameaga dunia akiwa jela kwa kukosa matibabu na uangalizi wa kitiba. Isiyaku alipigwa risasi na kujeruhiwa na jeshi la Nigeria mwezi Disemba mwaka jana alipokuwa katika hafla ya kidini huko Kaduna.

Kamisheni ya Kiislamu ya Haki za Binadamu ya nchini Nigeria imebainisha wasiwasi wake kuhusu hali ya usalama na matibabu ya wanachama wa harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo waliotiwa mbaroni.

Kamisheni ya Kiislamu ya Haki za Binadamu ya Nigeria Jumamosi ilitoa taarifa ikieleza inavyotiwa wasiwasi na hali za wanachama wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo walioko jela na kusisitiza kuwa, jeshi la Nigeria lingali linawauwa wanachama wa harakati hiyo ya Kiislamu na wafuasi wake.

Taarifa ya Kamisheni ya Kiislamu ya Haki za Binadamu ya Nigeria imeongeza kuwa imepokea taarifa za kuaminika kwamba wafungwa 14 ambao walilazwa katika hospitali ya jeshi katika jimbo la Kaduna baada ya kujeruhiwa vikali na jeshi la Nigeria hadi sasa hawajapatiwa matibabu yoyote.

Itakumbukwa kuwa, baina ya tarehe 12-14 Disemba Jeshi la Nigeria liliwashambulia wafuasi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria katika makaoa yao makuu mjini Zaria ambapo Sheikh Zakzaky alipigwa raisasi na kukammatwa huku mamia ya Waislamu wakiwemo wanawake na watutu wakiuawa katika mauaji ya kinyama.

3463904

captcha