IQNA

Mashindano ya Qur'ani Nigeria kuanza Januari 15

14:29 - January 07, 2016
Habari ID: 3470022
Mashindano ya 30 ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu ya Nigeria yatafanyika kuanzia Januari 15-23 katika jimbo la Nasarawa.

Taarifa kuhusu mashindano hayo imetolewa na Kituo cha Masomo ya Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Usmanu Danfodiyo jimboni Sokoto.

Akizungumza na waandishi habari, Dkt. Sani Yusuf Birin Tudu mratibu wa kitaifa wa mashindano hayo amesema awali ilikuwa imepangwa yaanzi Januari 8 lakini yakasongezwa mbele zaidi.

Waandalizi wa mashindano hayo wamebainisha masikitiko yao kufuatia kuahirishwa na kusema ilitokana na sababu ambazo hazingeweza kuepukika.

http://www.iqna.ir/en/news/3458679

captcha