IQNA

Waislamu waendelea kuandamana kulaani kuuawa Sheikh Nimr

13:44 - January 09, 2016
Habari ID: 3470026
Maelfu ya Waislamu katika nchi mbalimbali za duniani wamefanya maandamano makubwa ya kuulani jinai za utawala wa Saudi Arabia kufuatia utawala huo kumuua shahidi Sheikh Nimr Baqir al-Nimr, mwanazuoni mkubwa wa Kiislamu nchini humo.

Nchini Saudi Arabia Waislamu wa madhehebu ya Shia wameandamana katika mikoa ya Qatif na Al Ahsa kulaani kuuawa Sheikh Nimr ambaye alitoka eneo hilo la mashariki. Imearifiwa kuwa maandamano hayo yalifanyika kwa amani huku wananchi waliokuwa na hasira wakiulaani vikali utawala wa kiimla wa Aal Saud. Pamoja na kuwa maandamano yamekuwa yakifanyika kwa amani eneo hilo, vikosi vya kijeshi Ijumaa viliwashambulia waandamanaji kwa silaha na kumuua mtu moja.

Kwingineko nchini Iran Waislamu walimiminika mabarabarani katika miji yote baada ya sala ya Ijumaa na kulaani jinai za Aal Saud.

Waandamanaji hao sambamba na kusema kwa saudi kubwa: "Kifo kwa Marekani, kifo kwa Israel na kifo kwa Aal Saud," wamelaani vikali hatua zilizo dhidi ya binaadamu zinazofanywa na watawala wa Saudia katika eneo la Mashariki ya Kati hususan nchini Yemen, Syria na Iraq na kuutaja utawala huo kuwa ni kiini cha matatizo ya Waislamu duniani.

Mbali na Iran, maandamano makubwa kama hayo yamefanyika katika nchi mbalimbali ikiwemo Pakistan ambapo waandamanaji wamewalaani watawala wa Aal Saud, na kubeba mabango na picha za shahidi Sheikh Nimr Baqir al-Nimr. Aidha waandamanaji wamemtaja shahidi Sheikh Nimr kuwa mfano wa kuigwa na mwanamapambano mkubwa ambaye licha ya mashinikizo mbalimbali kutoka kwa utawala wa Saudia, hakurudi nyuma katika azma yake ya kutetea haki za raia wa nchi hiyo.

Wapakistan pia wameitaka serikali ya Islamabad kukata mara moja uhusiano wake na Saudia ambayo wameitaja kuwa ni nchi yenye utawala unaolea magaidi na kuwakandamiza Waislamu.

3465499

captcha