IQNA

Saudi Arabia yamkamata mwanazuoni wa Kiislamu Al Ahsa

17:48 - December 07, 2020
Habari ID: 3473433
TEHRAN (IQNA) - Mwanazuoni wa ngazi za juu wa madhehebu ya Kiislamu ya Kishia katika mkoa wa Al Ahsa katika mkoa wa mashariki mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa, maafisa wa usalama walivamia nyumba ya Allamah Sayyid Hashim al Shakhs Jumatatu na kumkamata.

Maafisa wa usalama walikuwa wamezingira mtaa anakoishi mwanazuoni huyo kabla ya kuivamia nyumba yake.

Al-Shakhs ni mwanazuoni maarufu Kiislamu na anayeshimika mashariki mwa Saudia.

Mamlaka husika nchini Saudi Arabia zimebomnoa msikiti mashuhuri wa Imam Hussein AS katika mji wa al-Awamiyah uliopo katika mkoa wa Qatif.

Hayo yanajiri wakati ambao mapema leo maafisa wa utawala wa Saudia wakiwa na maafisa wa ulinzi waliuzingira msikiti wa Imam Hussein AS na kuubomoa kikamilifu wakitumia buldoza.

Msikitu huo ndio mahala ambapo Shahidi Ayatullah Sheikh Baqir Nimr alikuwa akiswali na kutoa hotuba kabla ya kunyongwa na utawala huo wa kifalme.

Baadhi ya ripoti zinasema kuwa, watawala wa Saudia wamechukua hatua hiyo kutokana na chuki kubwa walizonazo ambapo wamekuwa wakifanya njama za kufuta athari zote za mwanazuoni huyo ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa watawala wa Aal Saud.

Ripoti zinasema kuwa, mpango wa kuubomoa msikiti huo uliandaliwa miezi kadhaa nyuma kwa kisingizio cha kupanua barabara.

Kwa mujibu wa uamuzi wa utawala wa Saudia, makumi ya nyumba pia katika barabara ya Thaura ambacho ni kitovu cha malalamiko na maandamano ya mji wa al-Awamiyah nazo zinapaswa kubomolewa.

Mji wa Qatif  wa mashariki mwa Saudia umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na wanajeshi wa Saudi Arabia na hadi sasa mamia ya wakazi wa mji huo wameuawa na wengine wengi kukamatwa kutokana na harakati zao za kisiasa.

Eneo hilo la mashariki mwa Saudia ndilo lenye utajiri mkubwa zaidi wa mafuta nchini humo lakini wakazi wa eneo hilo, ambao aghalabu ni Waislamu wa madhehebu ya Shia, wamekuwa wakikandamizwa na kudhulumiwa kwa muda mrefu sana.

3473337

Kishikizo: saudia AHSA shia al Shakhs
captcha