IQNA

23 wauawa katika hujuma ya magaidi Burkina Faso

15:54 - January 16, 2016
Habari ID: 3470050
Watu wasiopungua 23 wameuawa na karibu 15 wengine wamejeruhiwa katika kufuatia hujuma ya kigaidi katika hoteli moja nchini Burkina Faso, Ouagadougou.
Aidha askari wa Burkina Faso wamewakomboa makumi ya watu waliokuwa wametekwa nyara na watu wenye silaha katika hoteli ya Splendid ya mji mkuu wa nchi hiyo Ouagadougou.

Askari hao wa Burkina Faso wamepambana na watu hao wenye silaha katika hoteli hiyo na kuwakomboa watu 33.

Waziri mmoja wa serikali ya Burkina Faso ni miongoni mwa watu waliokoolewa kutoka mikononi mwa washambuliaji hao.

Alpha Barry, Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso amesema kuwa, watu wenye misimamo mikali ndio waliowavamia na kuwateka nyara watu hao.

Kundi la al Murabitun ambalo hivi karibuni lilijiunga na mtandao wa al Qaeda ndilo lililotangaza kuhusika na uvamizi huo wa hoteli hiyo Ijumaa usiku.

3467584


captcha