
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Sala hiyo imewajumuisha pamoja Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni ambao wamesali bega kwa bega. Waislamu wa Jamhuri ya Azerbaijan walioshiriki katika sala hiyo wamesisitiza kuhusu ulazima wa umoja na mshikamano baina ya Waislamu wa madhehebu za Kiislamu.
Mwaka 2016 umetajwa kuwa ni mwaka wa ‘Anuai za Tamaduni’ katika Jamhuri ya Azerbaijan ambapo Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni wanatumia fursa hiyo kusimamsiha sala pamoja.
Sala ya wiki hii imesaliwa katika msikiti wa Kishia na wiki Ijayo itasaliwa katika moja ya misikiti ya Kisunni.