Siku kama ya leo miaka 22 iliyopita yaani February 25 1994 Mzayuni mwenye uraia wa Marekani alihujumu Msikiti Palestina na kuua Waislamu 29.
Mzayuni huyo aliyekuwa na misimamo ya kufurutu ada aliwashambulia na
kuwamiminia risasi Waislamu waliokuwa wakitekeleza ibada ya Swala katika
Msikiti wa Haram ya Nabii Ibrahim mjini al Khalil, Palestina inayokaliwa kwa
mabavu na kuua shahidi 29 miongoni mwao. Mauaji hayo yalitokea wakati Waislamu
hao walipokuwa katika ibada ya funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Waislamu
wengine wengi walijeruhiwa katika shambulizi hilo la kikatili.