Katika hotuba iliyorushwa moja kwa moja na Televisheni ya Al Manar Jumanne usiku, Sayyid Hassan Nasrullah alisema: Kuna taarifa zinasambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinazodai kutokea mambo yasiyo sahihi katika baadhi ya maeneo ya Lebanon, lakini taarifa hizo zote ni za uongo, na hakuna matukio kama hayo yaliyotokea nchini Lebanon tarehe 7 Mei kama inavyodaiwa.
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameongeza kuwa, Saudia inachochea fitna za kimadhehebu kati ya Waislamu, suala ambalo limekuwa likifanywa kwa muda mrefu na utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani.
Amesema, harakati ya Hizbullah inalaani kitendo chochote cha kuvunjia heshima nembo za Kiislamu na kwamba suala hilo si kosa tu, bali ni dhambi.
Amesema kuna watu wanajaribu kuchochea fitna za kimadhehebu baina ya Waislamu kwa msaada wa kifedha wa Marekani, Saudia na Israel, na hiyo ni hatari kubwa sana kwa ulimwengu wa Kiislamu.