IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Hizbullah inakabiliana na maadui wa Waislamu

10:17 - March 19, 2016
Habari ID: 3470205
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amekosoa misimamo potovu ya baadhi ya nchi za Kiarabu dhidi ya Hizbullah ya Lebanon kwa kuitangaza harakati hiyo ya muqawama kuwa ni kundi la kigaidi.
Hizbullah inakabiliana na maadui wa WaislamuAyatullah Muhammad Ali Movahedi-Kermani ameeleza kwamba misimamo hiyo potofu inatangazwa katika hali ambayo kila mtu anakiri kuwa wanamapambano wa muqawama wa Lebanon wanailinda nchi hiyo na njama za utawala wa Kizayuni, makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Magharibi na baadhi ya tawala mbovu za eneo. Ameongeza kuwa Hizbullah inakabiliana na maadui wa Waislamu kote duniani.

Katika sehemu nyengine ya hotuba yake, Ayatullah Muhammad Ali Movahedi-Kermani amesema kuna ulazima wa vikosi vya ulinzi kujizatiti kwa silaha za kisasa kwa ajili ya kukabiliana na vitisho vya maadui.

Aidha ameashiria vitisho vya maadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kueleza kwamba katika mazingira kama hayo ni jambo la lazima kwa vikosi vya ulinzi kujizatiti kwa silaha; na suala hilo halina uhusiano na nchi yoyote.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amegusia ubabe na utumiaji mabavu unaofanywa na Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati na kusisitiza kuwa Marekani haiwezi kuizuia Iran isijizatiti kwa silaha za kisasa.

Aidha amelaani jinai zinazofanywa na utawala wa Aal Saud na utawala wa Kizayuni katika eneo hili na kuongeza kuwa Marekani inazipatia tawala hizo silaha zake angamizi ili zizitumie kwa ajili ya kuwaulia Waislamu.

Ayatullah Movahedi-Kermani amesema misimamo potofu ya Marekani katika Mashariki ya Kati ndio sababu ya machafuko na ukosefu wa amani unaoshuhudiwa katika eneo na akongezea kwa kusema, misimamo hiyo inasababisha madhara kwa nchi za eneo hili.

3459362

captcha