IQNA

Kongamano la Tadabbur au mazingatio katika Qur'an Tukufu kufanyika Malaysia

13:30 - May 31, 2016
Habari ID: 3470350
Kongamano la Kimataifa lenye anuani ya "Taddabur (Mazingatio) katika Qur'ani: Ubunifu na Ustawi" limepangwa kufanyika nchini Malaysia mwezi Novemba.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo litafanyika katika Akademia ya Sayansi za Kiislamu, Chuo Kikuu cha Malaya, Kuala Lumpur, nchini Malasia tarehe 15-16 Novemeba mwaka 2016.

Kitengo cha Qur'ani na Hadithi katika Akademia ya Sayansi za Kiislamu, Chuo Kikuu cha Malaya kimeamua kuandaa kongamano hilo kwa maudhui ya "Taddabur (Mazingatio) katika Qur'ani: Ubunifu na Ustawi" ili kuhimiza kuhusu uzingatiaji mafundisho ya Qur'ani Tukufu.

Kongamano hilo linatazamiwa kuangazia kwa kina kuhusu Taddabur katika ufahamu wa Qur'ani na maana ya aya za kitabu hicho kitukufu. Washiriki watajadili nnjia za kutatua matatizo ya ulimwengu wa sasa kwa kuzingatia aya za Qur'ani. Hali kadhalika washiriki watajadili namna watafiti Waislamu wanaweza kutumia ufahamu wa Qur'ani tukufu katika sekta mbali mbali za elimu na ubunifu.

Wasomi kutoka kote duniani wanaotaka kushiriki katika kongamano hilo wana hadi Julai 1, 2016 kuwasilisha muhtasari wa makala zao. Maelezo kamili yanapatikana katika tovuti ya:http://umconference.um.edu.my

3502660

captcha