Katika ujumbe wake huo uliotolewa Ijumaa hii, Kiongozi Muadhamu ameongeza kuwa: "Ni matarajio yangu kuwa mbali na kuwa mtajijenga kielimu, kidini na kiakhlaqi, muwe pia ni wenye taathira katika mazingira yenu na muongoze watu zaidi wafuate njia ya Mwenyezi Mungu kwa maneno na vitendo vyenu vyema."
Ayatullah Khamenei ameashiria kuwa, 'ujana na uanachuo' ni nukta zenye nguvuambazo humsaidia mwanadamu kufikia malengo yake ya juu' na kuongeza kuwa, 'mbali na kuwa muna sifa hizo mbili, pia mna sifa nyingine yenye taathira nayo ni kupitia jumuiya za Kiislamu.'
Kiongozi Muadhamu Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, kila moja anapaswa kunufaika na baraka za chemchemuya maarifa sahihi ya Kiislamu na kuwa katika njia nyofu ya Mwenyezi Mungu.