IQNA

Mamdani achaguliwa kwa kishindo kuwa meya wa kwanza Mwislamu wa New York

12:09 - November 05, 2025
Habari ID: 3481471
IQNA-Zohran Mamdani mbunge Muislamu amechaguliwa kuwa Meya wa 111 wa jiji la New York, mtu wa kwanza mwenye asili ya Asia Kusini na wa kwanza aliyezaliwa barani Afrika kuongoza jiji kubwa zaidi nchini Marekani.

Mamdani mwenye umri wa miaka 34 na mbunge kutoka Queens aliibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha jana kwa ajili ya kulioongoza jiji la New York baada ya kuhitimishwa upigaji kura katika mchuano mkali uliovutia hisia na fikra wa waliowengi.

Mamdani amemshinda mpinzani wake mkuu  gavana wa zamani Andrew Cuomo kwa kuibuka ushindi wa kura zisizopungua asilimia 50 kati ya jumla ya asilimia 85 ya kura zilizohesabiwa. 

"Tuko kwenye ukingo wa kuweka historia katika jiji letu. Katika ukingo wa kuaga siasa za zamani. Siasa ambazo zinakuamuru mambo yasiyotekelezeka." Ni matamshi ya Mamdani muda mfupi kabla ya kuibuka na ushindi. 

Mbunge huo Mdemocrat ameahidi kusimamia masuala ya kodi na usafiri wa mabasi bila malipo katika jiji la New York.

Takwimu zinaonyesha kuwa, msimamo wa Zohran Mamdani kuhusu Israel na Palestina umemsaidia pakubwa kuvuka katika mchuano wa awali wa kura kushutumiwa kutoa maoni ya kuwakosoa Wazayuni kuhusu vita na mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Gaza.

Kauli ya Trump

Mwitikio wa Trump

Kinyang’anyiro hiki kilijikita katika gharama ya maisha, usalama wa raia, na namna kila mgombea angekabiliana na Rais Donald Trump, ambaye alitishia kukata ufadhili wa serikali kuu kwa jiji la New York.

Mamdani alielekeza kampeni yake kwenye suala la maisha nafuu.

Ajenda yake inajumuisha kusitisha ongezeko la kodi ya nyumba kwa nyumba zilizo na udhibiti wa kodi, huduma ya basi bila malipo, huduma ya malezi ya watoto kwa wote, na maduka ya vyakula yanayoendeshwa na jiji.

Sera zake pia zinajumuisha kuongeza kodi kwa matajiri wa jiji la New York na kuinua kiwango cha kodi kwa makampuni, jambo lililozua hofu miongoni mwa wadau wa sekta ya fedha kuwa ushindani wa jiji unaweza kudorora.

Kupanda kwa Mamdani kwa njia isiyotarajiwa pia kunaangazia mjadala ndani ya Chama cha Democratic kuhusu iwapo kiendelee na msimamo wa wastani au wa mrengo wa kushoto.

Wakati huohuo, ushindi wa chama cha Democratic katika uchaguzi wa magavana wa Virginia na New Jersey ulionyesha mabadiliko ya hali ya kisiasa nchini Marekani, huku taifa likijiandaa kwa uchaguzi wa katikati ya muhula mwakani ambapo udhibiti wa Bunge la Congress utakuwa mashakani.

Trump, hata hivyo, alihusisha kushindwa kwa Warepublican katika jiji la New York, New Jersey, na Virginia na kutokuwepo kwake kwenye karatasi ya kura pamoja na kusitishwa kwa shughuli za serikali kuu.

Kulikuwa na hali ya huzuni miongoni mwa baadhi ya waliohudhuria hafla ya matokeo ya Cuomo, huku baadhi wakitabiri kuwa Trump angechukua hatua ya haraka kutuma Kikosi cha Ulinzi wa Taifa jijini New York.

 

3495280

Habari zinazohusiana
captcha