IQNA

Ayatullah Khatami katika Sala ya Ijumaa

Kama si Iran magaidi wa ISIS wangeteka Iraq, Syria na Lebanon

21:46 - March 03, 2017
Habari ID: 3470876
IQNA: Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amesisitiza kuwa, isingekuwepo misaada ya Iran, basi hadi kufikia sasa kundi la kigaidi la ISIS au Daesh lingekuwa limeziteka kikamilifu Iraq, Syria na Lebanon.

Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami ameongeza kuwa, lengo la Marekani na waitifaki wake la kuanzisha eneo ambalo nimarufuku kupaa ndege huko Syria si kuwaweka wakimbizi na kuongeza kuwa, Wamagharibi wanataka kuwapatia hifadhi magaidi katika eneo hilo kwa kuigawa nchi ya Syria.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo Tehran amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni ndugu mwenye nguvu wa nchi za Kiislamu za Mashariki ya Kati (Asia Magharibi) na kusema kuwa, uwezo wa Jamhri ya Kiislamu ya Iran ni katika njia ya uthabiti wa nchi hizo.

Ayatullah Khatami ameashiria kuongezeka propaganda za chuki dhidi ya Iran katika Mashariki ya Kati baada ya kuingia madarakani Rais mpya wa Marekani Donald Trump na kubainisha kwamba, watawala wa nchi za eneo wanapaswa kufahamu, Marekani inachotaka ni kuwatumia tu watawala hao kwa maslahi yake kama ilivyofanywa kwa dikta wa zamani wa Iraq Saddam Hussein na bila shaka iko siku itawaweka kando na kuachana nao.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran vile vile ameashiria kwamba, Marekani inafuatilia suala la kuzigawa nchi za Mashariki ya Kati na kubainisha kwamba, nchi za Mashariki ya Kati zinapaswa kuwa macho mbele ya fitina hizo za watawala wa Marekani.

3580158

captcha