IQNA

Rais wa Iran atuma ujumbe kwa munasaba wa kuadhimisha kuzaliwa Nabii Isa AS na kusema
10:45 - December 25, 2017
News ID: 3471323
TEHRAN (IQNA)-Rais Hassan Rouhani amemtumia salamu viongozi wa mataifa ya dunia na kuwapa mkono wa pongezi kwa mnasaba wa kuadhimisha kuzaliwa mtume wa rehma na saada Nabii Isa Masih AS na vilevile kwa kukaribia kuanza mwaka mpya wa 2018 miladia.

Mazungumzo, maelewano ya wanafikra yanaweza kuzia machafuko dunianiKatika salamu zake hizo, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, chini ya kivuli cha mafundisho ya Mitume wa Mwenyezi Mungu na kwa kushikamana na msingi wa kuishi kwa masikilizano, ana matumaini kwamba itawezekana kupiga hatua kubwa katika njia ya kueneza amani, uadilifu, usawa, udugu na kuwa na kadiri na wastani katika ufanyaji mambo.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa: Inapasa zifanyike jitihada, juhudi za pamoja, mazungumzo na maelewano kati ya wanafikra, maulamaa na wafuasi wa dini za Mwenyezi Mungu ili mwaka 2018 uwe mwaka uliojaa umaanawi, izza, ustawi wa jamii, kufutwa ubaguzi na kutoshuhudiwa machafuko kwa watu wote duniani.

Katika salamu nyengine alizomtumia Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis, Rais  Rouhani amesema: Chini ya kivuli cha mafundisho ya Mitume wa Mwenyezi Mungu na kwa kushikamana na tabia na mwenendo wao mwema nina matumaini kuwa katika mwaka mpya tutaweza kushuhudia kutokomezwa kila aina ya uchafu, maovu, ubaguzi na umasikini kwa wanadamu wote.

Leo Jumatatu, tarehe 25 Desemba inaadhimishwa kuwa ni siku aliyozaliwa Nabii Isa Masih AS.

3675883

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: