IQNA

Ujumbe wa Vatican watembelea Haram ya Imam Ali AS

20:52 - February 12, 2021
Habari ID: 3473645
TEHRAN (IQNA)- Ujumbe kutoka makao makuu ya Kanisa Katoliki Duniani, Vatican, umetembelea Haram Takatifu ya Imam Ali AS mjini Najaf, Iraq.

Ujumbe huo ukiongozwa na Mitja Leskovar, Balozi wa Vatican nchini Iraq  aliyekuwa akimuwakilisha Papa Francis, ulifika Najaf Alhamisi na kukutana na viongozi wa ngazi za juu wa Kiislamu kwa lengo la kujadili safari tarajiwa ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki nchini Iraq.

Ujumbe huo ulitembelea maeneo mbali mbali ya Haram ya Imam Ali AS  na kupata maelezo kuhusu yanayojiri katika eneo hilo takatifu alipozikwa Imam Ali AS.

Papa Francis anatazamiwa kutembelea Iraq Machi 5 kwa lengo la kukutana na viongozi wa nchi hiyo ya Kiarabu ambapo pia atakutana na kiongozi wa ngazi za juu wa Kiislamu Ayatullah Ali al-Sistani.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

3953540

captcha