IQNA

17:11 - May 05, 2018
News ID: 3471495
TEHRAN (IQNA) –Waislamu wa mji mkuu wa Australia, Canberra wana sababu ya kutabasamu kufuatia kufunguliwa msikiti mpya katika mji huo baada ya jitihahada za muda mrefu.

Mamia ya Waislamu walikusanyika Ijumaa katika ufunguzi wa Ahamd Al Sabah Masjid na Kituo cha Elimu ya Kiislamu baada ya jitihada za miaka mingi. Wakati msikiti wa kwanza ulipojengwa Canberra mwaka 1962, ulikuwa unaweza kuwahudumia waumini 300 tu lakini sasa idadi ya Waislamu mjini humo imeongezeka na kufika maelfu na hivyo kukawa na haja ya msikiti mpya hasa maeneo ya kusini.

Ujenzi wa Msikiti wa Ahmad Al Sabah, ambao sasa ni mkubwa zaidi Canberra, umekuwa ni jitihada za miongo kadhaa zilizojaa panda shuka, amesema Bi.Azra Khan mwanachama mwandamizi wa Kamati wa Kituo cha Kiislamu cha Canberra. 

Mwaka 2015 Waislamu wa Australia walikuwa wamefanikiwa kuchangisha kiasi kikubwa cha fedha lakini hawakuwa wamefikia kiwango walichohitajia hadi pale serikali ya Kuwait ilipotoa mchango wa dola milioni mbili ili kuwezesha msikiti kukamilika.

Balozi wa Kuwait nchini Austrailia Najeed al Bader amesema ni fahari yake kuwasaidia Waisalmu wa mjini Canberra huku akitaraji kuwa msikiti huo utakuwa na nafasi ya kueneza taswira bora na sahihi ya Uislamu.

3465717

 

Name:
Email:
* Comment: