IQNA

12:39 - April 29, 2019
News ID: 3471932
TEHRAN (IQNA) – Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kundi lenye misimamo mikali la Timu B linamchochea Rais Donald Trump wa Marekani aanzishe vita dhidi ya Iran.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mohammad Javad Zarif ameyasema  katika mahojiano aliyofanyiwa na televisheni ya Fox News ya Marekani na ambayo yamerushwa hewani kikamilifu Jumapili.

Zarif amesema katika mahojiano hayo kwamba John Bolton, mshauri wa usalama wa taifa wa Ikulu ya Marekani, White House, utawala wa Kizayuni, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) wanataka kuupindua utawala wa Kiislamu nchni Iran.  Ameongeza kuwa, timu "B" inayoundwa na Bolton, Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia na Bin Zayed mrithi wa kiti cha ufalme wa Imarati wanajaribu kuisukuma Marekani kuanzisha vita vya kijeshi dhidi ya Iran.

Zarif amesema vita vilivyoanzishwa na Donald Trump ambaye anasema ameiwekea Iran vikwazo vikubwa mno ambavyo havijawahi kushuhudiwa, vitashindwa tu.

Itakumbukwa kuwa baada ya kujitoa katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia JCPOA, serikali ya Donald Trump huko Marekani imeanzisha vita vya pande zote vya mashinikizo dhidi ya Iran.

3468386

Name:
Email:
* Comment: