IQNA

22:15 - July 01, 2019
News ID: 3472028
TEHRAN (IQNA) - Mcheza filamu maarufu India Zaira Wasim ametangaza kuondoka katika sekta ya utengenezaji filamu India maarufu kama Bollywood ili kujikurubisha zaidi kwa Allah SWT na kuhudumia Uislamu.

Bi.Wasim ambaye ana asili ya Kashmir, amepokeza zawadi kadhaa za uchezaji filamu nchini India. Aliance kucheza filamu mwaka 2016 alipoigiza nafasi ya mcheza mieleka katika filamu ya Dangal. Mwaka 2017 alipata Zawadi ya Kitaifa kwa Mtoto Mwenye Mafanikio Yasiyo ya Kawaida.
Katika ujumbe ambao aliutuma katika ukurasa wake rasmi wa Facebook, mcheza filamu huyo wa zamani Bollywood ambaye sasa ana umri wa miaka 18 amesema: "Miaka mitano iliyopita nilichukua uamuzi uliobadilisha maisha yangu. Niliopingia Bollywood, nilipata umashuhuri mkubwa." Anasema baada ya miaka mitano ya umashuhuri hajaridhika na hali hiyo kwani amekuwa na hisia kuwa huo si utambulisho wake wa asili. "Nilishanguliwa na kupata mashabiki katika tasnia hi lakini wakati huo huo hali hiyo ilisababisha nilikee katika njia ya ujahiliya (ujinga). Hatua kwa hatua na pasina kufahamu, niliondoka katika mkondo wa Imani ya Kiislamu," anasema Bi. Wasim. Anaongeza kuwa mazingira yake ya kikazi yalivuruga imani yake na hivyo akahisi uhusiano wake na Uislamu uko hatarini. "Nilijaribu kujiridhisha kuwa sikuwa nafanya kosa lolote lakini nilihisi maisha yangu hayakuwa na Baraka tena." Anaongeza kuwa, Baraka si kiwango kikubwa cha pato pekee bali pia ni uthabiti maishani ambao anasema aliupoteza.
Bi. Wasim anasema aliamua kufuata Qur'ani Tukufu na Sunna ya Mtume Muhammad SAW maishani.
Katika sehemu nyingine ya ukurasa wake wa Facebook ameandika: "Ewe Allah tuongoze tuweze kubaini baina ya haki na batili na tuwe na imani imara. Ewe Allah ondoa nifak, kibri, na ujahiliya na rekebisha nia zetu na tuwe na ikhlasi katika kauli na vitendo vyetu."

3468870

 

Name:
Email:
* Comment: