IQNA

14:03 - August 29, 2019
News ID: 3472105
TEHRAN (IQNA)- Washindi katika mashindano ya kitaifa ya kihifadhi Qur'ani wametunukiwa zawadi katika sherehe iliyofanyika Jumatano katika Ukumbi wa Kituo cha Kiutamaduni na Kiislamu cha mji w Gitega.

Kwa mujibu wa taarifa, mshindnao hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Kitabu na Sunna na kuhudhuriwa na wasichana na wavulana wapatao 50 kutoka kote Burundi.

Sheikh Khalid Abul Kafi, Naibu Katibu Mkuu wa JUmuiya ya Kimataifa ya Kitabu na Sunna amesema jumuiya hiyo imeandaa mashindano katika kategoria nne za kuhifadhi QUrani kikamilifu, kuhifadhi juzzu 15, kuhifadhi juzuu 10 na kuhifadhi juzuu 5.

Sherehe za kuwatunuku zawadi washindi zimehudhuriwa na viongozi wa kisiasa, wakurugenzi wa vituo vya Kiislamu na maimamu wa misikiti katika mji wa Gitega. Waliohutubu wamezungumzia kuhusu fadhila za kuhifadhi Qur'ani Tukufu huku wakiwahimiza washiriki kutekeleza mafundisho ya Qur'ani kivitendo.

Mashindano ya kitaifa ya Qur'ani Burundi

 

Mashindano ya kitaifa ya Qur'ani Burundi

Mashindano ya kitaifa ya Qur'ani Burundi

Mashindano ya kitaifa ya Qur'ani Burundi

Mashindano ya kitaifa ya Qur'ani Burundi

3838453

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: