IQNA

14:50 - April 03, 2020
Habari ID: 3472628
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Pakistan imetnagaza kusitishwa kwa muda sala za Ijumaa za jamaa kubwa kote nchini humo ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona.

Duru zimearifu kuwa serikali ya Pakistan imeamuru kuwa Sala ya Ijumaa isipindukie watu watano ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona au COVID-19 nchini humo.

Katika upande mwingine serikali ya Jimbo la Sindh imetangaza marufuku ya kutoka nje Ijumaa kuanzia saa sita hadi saa tisa mchana ili kuzuia watu kumiminika katika Sala ya Ijuma huku wananchi wakihimizwa kuswali katika majumba yao.

Wakati huo huo mwenyekiti wa Baraza la Itikadi ya Kiislamu nchini Pakistan Dakta Qibla Ayaz amesema kirusi cha corona kinawaathiri wafuasi wa madhehebu zote na ametaka kila atayakepoteza maisha kutokana na kirusi hicho atangazwa kuwa ni shahidi.

Aidha ametoa wito kwa watu wa Pakistan kuswali sala ya Ijumaa nyumbani ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona nchini humo. 

Nayo idara ya fatwa ya Dar ul Iftah Naeemia mjini Lahore, Pakistan imetoa fatwa na kusema watu ambao wanazuiwa na serikali kufika msikitini kuswali hawahajibiki kuswali sala za jamaa.

Hadi sasa watu 2,450 wameambukizwa corona nchini Pakistan huku wengine 35 wakipoteza maisha kutokana an ugonjwa huo hatari.

3471021

 

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: