IQNA

Janga la Corona

Wafuasi 20,000 wa Tabligh Jamaat wawekwa karantini Pakistan baada ya kushiriki ‘Ijtimai’

12:09 - April 08, 2020
Habari ID: 3472646
TEHRAN (IQNA) – Pakistan imewaweka katika karantini watui 20,000, na inawasaka maelifu yaw engine, walioshiriki katika mjumuiko wa Waislamu ambao ni maarufu kama Ijtimai katika mji wa Lahore mwezi uliopita, huku janga la COVID-19 au corona likiendelea kuwa mbaya nchini humo.

Maafisa wa Pakistan wanasema wanataka kuwapima au kuwaweka katika karantini wote walioshiriki katika mjumuiko huo ambao uliandaliwa na harakati ya kuutangaza Uislamu ya Tabligh Jamaat.  Ijtimai hiyo ilifanyika Machi 10-12 na kuna wasiwasi kuwa walioshiriki wanaeneza ugonjwa wa COVID-19 ndani na nje ya Pakistan.

Taarifa zinasema walioshiriki katika Ijimai hiyo wanakadiriwa kuwa 100,000 na walishiriki katika kikao hicho kwa kukaidi ombi la serikali la kuzuia mijumuiko baada ya ugonjwa wa corona kuripotiwa nchini humo.

Katika jimbo la Khyber Pakhtunkhwa, la kaskazini mashariki mwa Pakistan, wanachama 5,300 wa Tabligh Jamaat walioshiriki kikao cha Lahore wamewekwa katika karantini.

"Maafisa wa usalama  wanawapima ugonjwa wa COVID-19 na baadhi wamepatikana na ugonjwa huo," amesema Ajmla Waziri, msemaji wa jimbo hilo.

Wazir amesema maelfu ya wafuasi wa Tabligh Jamaat kutoka mkoa huo wamekwama maeneo mengine ya Pakistan kwa sababu barabara muhimu zimefungwa kuzuia kuenea corona. 

Harakati ya Tabligh Jamaat ni moja ya harakati kubwa zaidi za kidini duniani na ina mamilioni ya wafuasi hasa eneo la Kusini mwa Asia na hutuma wahubiri maeneo mbali mbali ya dunia kuutangaza Uislamu.

Hadi sasa watu zaidi ya 4,000 wameambukizwa COVID-19 nchini Pakistan huku wengine wasiopungua 54 wakipoteza maisha.

3890001

captcha