Katika video hii, Sheikh Tariq anasoma aya ya 185 ya Surah al-Baqara ya Qur’ani Tukufu isemayo: “ Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru.”
Taqriq ni kati ya watoto 10 wa marhum Sheikh Abdu Basit. Katika mahojiano aliyowahi kufanya huko nyuma alisema baba yake alisisitiza kuwa yeye na ndugu zake wote wahifadhi Qur’ani Tukufu. Tariq alihifadhi Qur’ani kikamilifu akiwa na umri wa miaka 15 na baada ya hapo akawa qarii mashuhuri kama alivyokuwa baba yake.