Kwa mujibu wa tovuti ya youm7, Sheikh Shahat Mohammad Anwar ambaye ni kati ya wasomaji Qur’ani (qarii) mashuhuri Misri na ulimwengu wa Kiislamu alizaliwa 29 Mei mwaka 1978 katika eneo la Mit Ghamr mkoani El Dakahila nchini Misri.
Akiwa bado mototo mdogo alihifadhi Qur’ani Tukufu kwa msaada wa baba yake na baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Al Azhar na kuhitimu katika taalauma ya fasihi ya Kiarabu.
Qarii huyu kijana kutoka Misri mnamo mwaka 2004 alipita mtihani na kuweza kuidhinishwa kuwa qarii rasmi wa Radio ya Misri.