TEHRA (IQNA) – Klipu ya video imesmabazwa hivi karibuni ya qiraa ya Surah Al-Infitar ya Qur'ani Tukufu ya marhum Sheikh Abdul-Basit Abdul-Swamad.

Katika klipu hiyo ambayo haijatajwa tarehe yake anasikika akisoma aya za 6-8 za Surah Al-Intifar zisemazo: " Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu? Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha. Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga."