IQNA

16:30 - May 26, 2020
News ID: 3472805
TEHRAN (IQNA)- Mahmoud Abdul Fattah Taruti, anafuata nyayo za baba yake, Ustadh Abdul Fattah Ali Taruti, mmoja wa wasomaji mashuhuri wa Qur'ani nchini Misri.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 16 ana sauti nzuri na ni stadi katika Tajwid na usomaji jumla wa Qur'ani Tukufu.

Mahmoud anaishi katika kijiji cha Tarut katika jimbo la Sharqia nchini Misri na anaendelea na masomo katika shule ya upili huku akiwa na azma ya kusomea udaktari katika chuo kikuu.

Mahmoud anasema alianza kuhifadhi Qur'ani akiwa na umri wa miaka mitano na alifanikiwa kuhifadhi kikamilifu  akiwa na umri wa miaka 13. Aidha amejifunza mbinu za qiraa ya Qur'ani Tukufu na sasa yeye husoma katika Radio ya Qur'ani nchini Misri.

Tizama au sikiliza qiraa ya Mahmoud Abdul Fattah Taruti hapa chini.

3901343

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: