IQNA

Wakuu wa Saudia watafakari kuanzisha tena Ibada ya Umrah

21:51 - September 14, 2020
Habari ID: 3473167
TEHRAN(IQNA)- Saudi Arabia inatafakari kuanzisha tena Ibada ya Umrah baada yakuisitisha kwa miezi kadhaa sasa.

Umrah ilipigwa marufuku Saudia mwishoni mwa mwezi Februari kama mojawapo ya hatua ambazo zilichukuliwa kuzuia kuenea ugonjwa wa umrah.

Hivi sasa Saudia inapanga kuruhusu safari chache za ndege za kimataifa kutoka na kuingia nchini humo kuanzia Septemba 15.

Shirika rasmi la habari la Saudia SPA limenukulu duru za Wizara ya Ndani zikisema kuna uwezekano wa kuanza tena Ibada ya Umrah.

Hadi sasa watu 325,000 wameambukizwa corona nchini Saudia na migongoni mwao 4,200 wamefariki dunia.

3472556

Kishikizo: umrah ، saudi arabia ، corona
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :