IQNA

16:00 - September 25, 2020
News ID: 3473202
TEHRAN (IQNAQ)- Waislamu nchini Ujerumani watawakaribisha wasiokuwa Waislamu katika misikiti mnamo Oktoba 3 katika siku hii ambayo kila mwaka inajulikana kama ‘Siku ya Msikiti Wazi.’

Sikuu hii ambayo pia ni siku ya kuungana tena Ujerumani  hutumika kama nembo ya kujumuka Waislamu wa Ujerumani katika utamaduni wa nchi hiyo. Kwa msingi huo siku hiyo pia inaashiria pia mshikamano na kuheshimiana watu wa Ujerumani.

Misikiti ambayo inashiriki katika mpango huo, mbali na kuwakaribisha watu wa matabaka mbali mbali  kutembea na kuona msikiti pia itaandaa mihadhara na maonyesho ya kuelimisha kuhusu Uislamu. Aidha wageni watakaofika msikiti wataandaliwa chakula kutoka jamii mbali mbali za Waislamu wanaotaka Kusini mwa Asia, Afrika, eneo la Balkan na Asia Magharibi.

Mpango huo umeandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Ujerumani na misikiti zaidi ya 1,000 itashiriki na na kwa kawaida karibu wageni 10,000 hutembelea misikiti. Mwaka huu kutokana na janga la corona inatarajiwa idadi haitakuwa kubwa sana.

Kuna Waislamu zaidi ya milioni 4 nchini Ujerumani na wengi walizaliwa na kulelewa nchini humo huku wengine wakiwa wamewasilia miaka ya karibuni kama wakimbizi.

3925222

Tags: ujerumani ، waislamu ، msikiti
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: