IQNA

Misikiti yafunguliwa Ujerumani baada ya miezi miwili

9:20 - May 10, 2020
Habari ID: 3472751
TEHRAN (IQNA) – Misikiti nchini Ujerumani imefunguliwa Jumamosi baada ya kufungwa kwa muda wa miezi miwili kutokana na janga la ugonjwa wa COVID-19 au corona.

Kwa mujibu wa taarifa waumini walianza kuingia misikitini Jumamosi alfajiri kwa kuzingatia kanuni za kiafia ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa au maski, visafishi au sanitiza na kuzingatia umbali wa mita 1.5 wakati wa Swala.

Ujerumani imeanza kupunguza zuio la kutoka nje ambalo lilikuwa linatekelezwa nchini humo kuzuia kuenea corona.

Serikali ya Ujerumani imeruhusu shule, misikiti, makanisa na viwanja vya michezo kufunguliwa hatua kwa hatua kwa sharti la kuzingatia kanuni za afya za kukabiliana na COVID-19.

Hadi sasa Ujerumani imeripoti kesi 170,000 za maambukizi ya COVID-19 ambapo watu 7,500 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo hadi kufikia Mei 10.

3897493


مساجد آلمان بازگشایی شدند/ در حال تکمیل

مساجد آلمان بازگشایی شدند/ در حال تکمیل

مساجد آلمان بازگشایی شدند/ در حال تکمیل

مساجد آلمان بازگشایی شدند/ در حال تکمیل

مساجد آلمان بازگشایی شدند/ در حال تکمیل

مساجد آلمان بازگشایی شدند/ در حال تکمیل

مساجد آلمان بازگشایی شدند/ در حال تکمیل

مساجد آلمان بازگشایی شدند/ در حال تکمیل

captcha