IQNA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen

Marekani, Uingereza, Saudia na UAE ni watenda jinai katika eneo

20:02 - October 10, 2020
Habari ID: 3473246
TEHRAN (IQNA) - Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya uokovu wa kitaifa ya Yemen amesema Marekani, Uingereza, Saudia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ni watenda jinai katika eneo zima la Ghuba ya Uajemi.

Hisham Sharaf amesema madola hayo ni mhimili wa sharti katika eneo na badala ya kuhitimisha hujuma yao dhidi ya Yemen huitisha vikao visivyo na maana vya masuala ya 'kibinadamu' na kiuchumi.

Ameongeza kuwa Saudi Arabia na UAE ni wahusika na wasababishaji wakuu wa moja ya hali mbaya zaidi ya maafa ya kibinadamu katika historia.

Hisham Sharaf ameeleza kuwa, muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudia ndio unaobeba dhima ya kuteketezwa na kuangamizwa Yemen na wala hauwezi kujivua na kuhepa mzigo wa adhabu na ubebaji gharama za uharibifu na uteketezwaji wa nchi hiyo.

Wakati huohuo Talaat Ash-Sharjabi, msemaji wa Baraza Kuu la masuala ya kibinadamu la Yemen amekosoa uamuzi wa kulitunukia Tuzo ya Amani ya Nobeli Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP na kueleza kwamba, WFP haijawahi kuonyesha msimamo na muelekeo wa kutopendelea upande wowote; na umekuwa na taksiri katika kutekeleza majukumu yake kuhusiana na uhaba wa chakula na lisheduni inayowakabili watu wa Yemen.

Ikumbukwe kuwa mnamo mwezi Machi 2015 Saudi Arabia, ikiungwa mkono na  Marekani, Imarati na nchi zingine kadhaa iliivamia kijeshi Yemen na kuiwekea mzingiro wa kila upande nchi hiyo. Moto wa vita uliowashwa na Saudia na waitifaki wake nchini Yemen hadi sasa umesha sababisha makumi ya maelfu ya watu kuuawa na mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi.

Uvamizi wa kijeshi wa Saudia umeisababishia pia nchi masikini ya Yemen uhaba mkubwa wa chakula na dawa.

3928348

captcha