IQNA

Uturuki yasambaza nakala milioni moja za Qur’ani katika nchi 80

20:41 - January 05, 2021
Habari ID: 3473527
TEHRAN (IQNA) - Idara ya Masuala ya Kidini Uturuki (Diyanet) imesambaza nakala milioni moja za Qur’ani katika nchi mbali mbali duniani.

Ehsan Ajiq, naibu mkuu wa Idara ya Masuala ya Kidini Uturuki ametangaza  Jumanne kuwa misahafu hiyo imesambazwa katika fremu ya kampeni ya  ‘Zawadi Yangu Inapaswa Kuwa Qur’ani Tukufu’ ambayo ilianzishwa mwaka 105. Katika fremu ya kampeni hiyo misahafu milioni moja imesambazwa katika nchi 80 duniani.

Ajiq ameongeza kuwa wamejitahidi kuhakikisha kuwa ujumbe wa Qur’ani Tukufu unawafikia watu katika kona zote za dunia. Aidha amesema nakala za Qur’ani ambazo wanasamabza pia zina tarjuma ya lugha 20 za maeneo muhimu ya dunia.

3945982

captcha