IQNA

Utamaduni

Maktaba Riyadh yazindua maonyesho ya Misahafu iliyopambwa

15:34 - March 17, 2024
Habari ID: 3478529
IQNA - Maktaba ya Umma ya Mfalme Abdulaziz mjini Riyadh imezindua maonyesho yenye nakala 42 za Qur'ani 42 ambazo kila moja imeandikwa kwa kaligrafia ya Kiislamu na mapambo ya aina yake.

Maonyesho hayo yaliyofunguliwa Alhamisi, yameundwa kuambatana na sherehe za kitaifa na kidini na pia yatawasilishwa kimataifa, kulingana na Asharq Al-Awsat.

Faisal bin Muammar, msimamizi mkuu wa maktaba hiyo, alisema kuwa mkusanyiko huo unatoa mfano wa mageuzi ya sanaa ya Kiislamu kupitia aya za Qur'ani.

Alibainisha ushawishi mkubwa wa tamaduni za kisanii za Kiislamu kwenye aina za sanaa za kimataifa, ikiwa ni pamoja na sanaa ya Magharibi, kupitia njia kama vile maandishi ya kaligrafia na mapambo yanayopatikana katika kazi za mikoni  kama vile nguo, vyombo vya kioo na ufinyanzi.

Bin Muammar aliangazia umuhimu wa kaligrafia na mapambo katika Qur'ani, ambavyo alivielezea kuwa ni nembo ya utambulisho wa kitamaduni na umoja wa ulimwengu wa Kiislamu.

Maktaba hiyo ina zaidi ya Misahafu au nakala za Qur'ani zipatazo  350 ambazo ni za aina yake kwani ziliandikwa kwa mitindo tofauti katika historia ya Kiislamu.

captcha